Uhaba wa maji wakumba Lagdera baada ya Vidimbwi kukauka

Wakazi wa kaunti ndogo ya  Lagdera kaunti ya  Garissa wametoa wito kwa serikali kushughulikia tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo.

Wakazi hao wamesema wakati mwingine wanalazimika kununua mafuta ya malori ya maji ya serikali ya kaunti na kulipa madereva marupurupu ili waweze kupata maji.

Kulingana na afisa wa idara ya maji katika eneo hilo  Feisal Ali, kaunti ndogo nzima ya Lagdera ina lori moja pekee la kusambaza maji kwa wakazi kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo .

Akiongea katika mji wa  Modogashe baada ya kukutana na kamishna wa kaunti hiyo Boaz Cherutich, wakazi hao wanesema wamekuwa wakikosa maji tangu msimu wa ukame ulipoanza miaka miwili iliyopita.

Cherutich amesema tatizo hilo linatokana na hali ya kukauka kwa vidimbwi vya maji na ung’ang’aniaji wa maji kati ya binadamu na mifugo.  

Hata hivyo Cherutich ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo na shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia watoto  UNICEF, kukarabati visima vyote vya maji na malori ya maji ili kuwezesha kurejelewa kwa usambazaji wa maji kwa wakazi.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi