Uhuru Kenyatta: Kenya imepiga hatua katika sekta ya afya tangu Uhuru

Rais  Uhuru Kenyatta ameelezea hatua iliopigwa katika mpango wa afya kwa wote  ambao ni mojawapo wa  ajenda nne kuu, akisema ugonjwa wa  Covid-19 umepelekea kuimarishwa  kwa sekta ya afya.  

Rais alitumia fursa hiyo kuwapongeza wahudumu wa afya kwa kujitolea licha  ya changamoto kubwa ya afya  kuwahi kukabili taifa hili kwa miaka nyingi.

Also Read
Nyanza yaongoza kwa ukusanyaji saini kuunga mkono BBI

Amesema ingawaje kungali kuna changamoto mbali mbali, ni lazima ijulikane kwamba kuimarisha sekta ya afya hadi viwango vinavyohitajika  ni jukumu linaloendelea kutekelezwa na serikali.

Also Read
Biden atenga dola trilioni 1.9 kukabiliana na Covid-19

Akihutubia taifa wakati wa maadhimisho ya miaka 57 ya siku kuu ya Jamhuri katika uwanja wa michezo wa  Nyayo, rais  Kenyatta alisema serikali yake imefanikiwa kuweka vifaa vya matibabu kwa muda mfupi zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu taifa hili kujinyakulia uhuru.

Also Read
Rais Kenyatta awarai wawekazi wa Ufaransa kuchagua Kenya kwa uwekezaji wao

Kwa mujibu wa Rais kituo cha kutibu saratani cha hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta sasa kimekamilika  na sasa wakenya hawana haja ya kusafiri nje kwa matibabu maalum ya saratani.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi