Uingereza kushikana mashati na Denmark Jumatano kuwania fursa ya kupiga na Italia fainali ya Euro

Uingereza itashuka uwanjani Wembley jijini London ,dhidi ya Denmark katika nusu fainali ya mwisho ya kombe la Euro Jumatano usiku kuanzia saa nne usiku .

Mechi hiyo itahudhuriwa na mashabiki elfu 60 zaidi ya robo tatu wakiwa wa Uingereza.

Timu hizo zitakutana kwa mara ya 24 leo katika mechi za kimataifa Waingereza wakishinda 13 ,Denamark wakaibuka kidedea mara tano huku mechi 5 zikiishia sare.

Also Read
Gor kuanza kutetea ubingwa dhidi ya wagema mvinyo Tusker Fc
Uingereza wakiwa mazoezini

Katika uwanja wa Wembley Denmark imecheza mechi 7 wakishinda au kupoteza kwa bao 1-0 ,mara ya mwisho kuzima kidomodomo cha mwingereza nyumbani kufuatia ushindi wa bao 1-0 ikiwa Oktoba 14 mwaka jana katika mechi ya Uefa nations league.

Also Read
Chelsea kuvaana na Mancity fainal ya ligi ya mabingwa Ulaya Mei 29

Denmark watakuwa wakiwania kombe la pili la Euro baada ya kuibuka mabingwa mwaka 1992.

Denmark baada ya ushindi dhidi ya Czech

Uingereza haijawahicheza fainali ya kombe la euro ,ikishindwa katika nusu fainali mara mbili mwaka 1968 na 1996 wakati Denmark waliotawazwa mabingwa mwaka 1992 wakishiriki nusu fainali ya euro kwa mara ya nne wakipoteza mara mbili .

Also Read
Mzunguko wa kwanza wa mechi za makundi Kipute cha Euro kukamilika Jumanne

Uingereza imesawazisha rekodi ya Uhispania mwaka 2012 walionyakua kombe hilo , kushinda mechi 5 bila kufungwa bao .

Mechi hiyo itang’oa nanga saa nne usiku huku mshindi akipambana na Italia katika fainali ya Jumapili kiwarani Wembley .

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi