Uingereza yaboresha uwezo wa Kenya wa kutambua aina mpya za Virusi

Kenya itapokea usaidizi wa vifaa vya uchunguzi kupitia mfumo mpya wa serikali ya Uingereza kuhusu uchunguzi wa aina mpya za virusi (NVAP), kama sehemu ya mpango wa ushirikiano kati ya Kenya na Uingereza.

Mfumo huo utatoa fursa kwa uwezo wa kipekee wa Uingereza katika kuchunguza na kukadria virusi, kupiga jeki juhudi za Kenya katika kupambana na janga la Covid-19, na kuboresha usalama wa ki-afya kote duniani.

Also Read
Watu 277 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona

Usaidizi huo unajumuisha kemikali na vifaa vya kuwachunguza wasafiri wanaoingia humu nchini, ushauri wa kiufundi, na pia mafunzo.

Ushirikiano huo utakuwa kati ya taasisi ya KEMRI hapa nchini na Idara ya Afya ya umma ya Uingereza na utachangia mpango wa ushirikiano katika sekta ya afya  uliotiwa saini kati ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza Dominic Raab na waziri wa afya Mutahi Kagwe, wakati wa ziara ya waziri huyo hapa nchini Kenya mwezi Januari mwaka huu.

Also Read
Kenya yanakili visa 123 vipya vya Covid-19

Waziri wa afya Mutahi Kagwe alikaribisha usaidizi huo akisema utasaidia pakubwa kukabiliana na janga hili na pia zile zitakazoibuka katika siku zijazo.

“Nina furaha kupeleka uhusiano wa sekta ya afya kati ya Kenya na Uingreza katika kiwango kingine. Kupitia taasisi ya utafiti wa kimatibabu KEMRI na chuo kikuu cha Oxford, tuna ushirikiano wa miaka 30 unaoendelea kukua tunapopanua wigo wetu katika sekta ya afya,” alisema Kagwe.

Also Read
Ann Nderitu: Vyama vya kisiasa viko huru kujiondoa kwa miunganano ya vyama

Balozi wa uingereza Jane Marriot alisema janga la Covid-19 limeboresha uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

“Wanasayansi wa KEMRI na wenzao wa chuo kikuu cha Oxford walihusishwa katika utengenezaji wa chanjo ya AstraZeneca,” alisema Marriot.

  

Latest posts

Wanamichezo 11 wapokea msaada wa masomo kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini NOCK

Dismas Otuke

Watu wawili wafariki baada ya jengo kuporomoka Kiambu

Tom Mathinji

TIFA: Uwaniaji Urais wa Raila-Karua ni maarufu zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi