Uingereza yalegeza masharti ya Covid-19 kwa wasafiri wa Ufaransa

Watu waliopata chanjo kikamilifu sasa wanaweza kuzuru Ufaransa bila kukaa karantini wanaporejea nchini Uingereza, baada ya mabadiliko ya kanuni za usafiri kuanza kutekelezwa.

Kampuni ya meli ya Brittany ya ufaransa ilisema maombi ya usafiri yameongezeka kufuatia mabadiliko hayo yaliyotangazwa siku ya Alhamisi.

Also Read
Bush ampongeza Biden kwa ushindi wa kura za Urais Marekani

Hata hivyo kampuni za uchukuzi zimesema kuwa hatua hiyo ya kulegeza kanuni za karantini kwa eneo maarufu zaidi la kuzuru kutoka uingereza imechelewa kwani idadi kubwa ya watu husafiri wakati wa majira ya joto.

Also Read
Wanajeshi wa Marekani wamekaribishwa Somalia, asema Rais Hassan Sheikh Mohamud

Kuambatana na mabadiliko kwa mfumo wa uchukuzi nchini uingereza, kanuni hizo zimelegezwa kwa nchi kadhaa.

Ufaransa ililegeza kanuni zake na kupunguza kiwango cha hatari ya maambukizi ambapo watoto na wasafiri waliopata chanjo kikamilifu hawatahitajika kukaa karantini wanaporejea.

Also Read
Japan kusitisha juma hili hali ya hatari iliyowekwa kudhibiti Covid-19

Hata hivyo,  wasafiri ambao hawajapata chanjo ni sharti wajitenge nyumbani kwa siku 10.

  

Latest posts

Watu 20 wauawa na wanamgambo katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo

Tom Mathinji

Rais Joe Biden apona virusi vya Covid-19

Tom Mathinji

Manara na Hersi Matatani

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi