Uingereza yazidisha masharti ya kudhibiti Corona

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameweka masharti makali zaidi na kubatili mipango ya kulegeza masharti ya kuzuia msambao wa COVID-19 wakati wa maadhimisho ya Krismasi.

Idadi ya visa vya maambukizi nchini Uingereza imeongezeka katika muda wa wiki mbili zilizopita kutokana na aina mpya ya virusi vya Corona ambavyo Wanasayansi wanasema kusambaa kwake kutakuwa asilimia 70 zaidi.

Also Read
Raia wa Kenya wapigwa marufuku kuingia nchini Uingereza

Ijapo Johnson na washauri wake wa masuala ya Sayansi bado wanaamini kutakuwa na ufanisi kutokana na chanjo, na kwamba aina mpya ya virusi vya Corona sio hatari zaidi kuambatana na magonwja, Waziri Mkuu huyo amesema serikali yake haina budi kuchukua hatua.

Also Read
Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi Uturuki yafika watu 27

Maeneo ya Jiji la London na pia Kusini-Mashariki mwa Uingereza – ambayo ni nyumbani kwa thuluthi moja ya raia wote wa Uingereza – kwa sasa yanashuhudia masharti makali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

Also Read
Kenya yapokea dozi 880,460 aina ya Moderna kukabiliana na COVID-19

Wakazi watahitajika kubakia nyumbani ila kuwe na sababu maalum kama zile za kikazi, na pia maduka yasioyouza bidhaa muhimu yatafungwa, sawia na kundi na vituo vya burudani.

  

Latest posts

Shule nchini Uganda kufunguliwa Januari mwaka 2022

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi