Unyakuzi wa ardhi watatiza ukarabati wa barabara ya Thika

Kuvamiwa kwa maeneo ya upanuzi wa barabara na wanyakuzi wa ardhi na ujenzi wa milingoti ya umeme kwenye maeneo hayo imesemekana ndivyo vizingiti vikuu kwa mradi wa shilingi bilioni moja wa kuweka lami kwenye barabara ya Thika.

Benjamin Asin ,ambaye ni naibu wa mkurugenzi wa mamlaka ya barabara za mijini-KURA, amesema ni aslimia 1 tu ya kazi kwenye barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 17 ya Gatuanyaga,katika kaunti ndogo ya Thika Mashariki iliyoanza mapema mwezi huu ambayo imekamilishwa.

Alisema kwa sasa wanawafuatilia wahusika kubomoa mabanda yaliojengwa katika sehemu hiyo ya ujenzi wa barabara,huku akisema watakaokataa,mabanda yao yatabomolewa kwa nguvu.

Wakati uo huo Asin ameitaka kampuni ya uzalishaji umeme ya Kenya Power kuihamishia kwingineko milingoti yake ya umeme ambayo ipo kwenye eneo la ujenzi wa barabara hiyo.

Mbunge wa Thika Patrick Wainaina aliyeandamana na wahandisi wa KURA kukagua ujenzi wa barabara hiyo, alisema anatarajia ujenzi huo utakamilika kwa muda uliowekwa.

Aliwaonya walionyakua ardhi uliotengewa upanuzi wa barabara kuwa huenda wakapoteza fedha zao.

Barabara hiyo itayoyoma kutoka Gatuanyaga-Muguka-Ngurai-Munyu-Gitima- Kang’oki hadi Kisii na ni ya daraja la B,ambayo ina uwezo wa kustahimili malori ya uzani mkubwa yanayofanya kazi ya kusomba mchanga na mawe katika sehemu hiyo.

  

Latest posts

Ruto: Mawakala wa kisiasa waliboronga uhusiano wangu na Rais Kenyatta

Tom Mathinji

COTU yazusha kuhusu nyongeza ya bei za mafuta nchini

Tom Mathinji

John Munyes na Charles keter kufika mbele ya Senate kuhusu ongezeko la bei ya mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi