Upigaji kura katika maeneo bunge ya Bonchari na Juja waendelea

Shughuli ya upigaji kura kwenye uchaguzi mdogo inaendelea katika maeneo bunge ya Bonchari na Juja  mtawalia.

Chaguzi hizo zinanuiwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufwatia vifo vya wabunge wa maeneo hayo.

Kiti cha ubunge cha Bonchari kimewavutia wagombea 13, wakiwemo Zebedeo Opore wa chama cha Jubilee,Pavel Oimeke wa chama cha ODM na mjane wa aliyekuwa mbunge wa sehemu hiyo John Oyioka na Teresa Bitutu wa chama cha UDA miongoni kwa wengine.

Also Read
Mwanaume akamatwa kwa kuwabaka binti wake wawili

Nacho kitu cha eneo bunge la Juja kina mezewa mate na takriban wagombea 11 ambao wanajumuisha mwaniaji kwa tiketi ya chama cha Jubilee Susan Njeri Waititu,George Koimburi wa Peoples Empowerment Party na Joseph Kariuki Gichui ambaye ni mgombea wa kujitegemea miongoni kwa wengine.

Also Read
Shughuli za Kampeini zasitishwa katika maeneo bunge ya Bonchari na Juja

Kati ya wagombea 11 wa  kiti cha ubunge cha Juja, watano ni wagombea wa kujitegemea.

Viti vya ubunge vya Bonchari na Juja viliachwa wazi kufwatia vifo vya John Oyioka na Francis Waititu mtawalia.Oyioka aliaga dunia  katika hospitali moja mjini Kisumu baada ya kuugua kwa muda mrefu,huku Waituti akiaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya ubongo.

Also Read
IEBC yashtumiwa kwa kuajiri wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa Bonchari kutoka maeneo mengine

Uchaguzi huo unaendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka chini ya sheria na kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Visa 511 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi