Usalama waimarishwa Bonchari kabla ya uchaguzi mdogo wa Jumanne

Mratibu wa eneo la Nyanza, Magu Mtindika, amewahakikishia wakaazi wa eneo bunge la Bonchari kuhusu usalama wao, wakati wa uchaguzi mdogo siku ya Jumanne juma lijalo baada ya kupeleka maafisa wa kutosha wa usalama katika eneo hilo.

Akiwahutubia wanahabari kwenye afisi ya Kamishna wa kaunti mjini Kisii, Mtindika alisema polisi wamewatia nguvuni na kuwafikisha mahakamani watu watatu kwa tuhuma za kuvuruga amani, ilhali wengine watafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Aliongeza kwamba polisi wana majina ya wamiliki wa magari mawili yaliyokuwa yamesheheni mapanga na silaha nyingine butu, ambazo yaaminika zingetumiwa kuzua vurugu mnamo siku ya uchaguzi.

Also Read
KPA yatahadharisha kuhusu hali mbaya ya hewa Pwani kutokana na kimbunga cha Jobo

Aliagiza kamanda wa polisi kuwakamata watu hao na kuwafikisha mahakamani siku ya Jumatatu.

Katika jawabu lao, vyama vya UDA na ODM vilidai polisi wanawadhulumu na kuwangaisha wawaniaji na pia wafuasi wao.

Mtindika aliwatetea maafisa wa polisi kwa kusema kwamba wanatekeleza majukumu yao ya kuhakikisha sheria na utangamano vinadumishwa.

Uchaguzi mdogo was kiti cha eneo bunge la Bonchari utafanyika siku ya Jumanne juma lijalo, kujaza nafasi iliyoachwa na Oroo Oyioka, ambaye alifariki miezi mitatu iliyopita.

Also Read
Mbunge wa Bonchari Oroo Oyioka aaga dunia

Katika eneo bunge la Juja, Kamishna wa Kaunti ya Kiambu, Wilson Wanyanga, amesema hatua za usalama pia zimewekwa kuhakikisha wapiga kura wanatekeleza haki zao za kidemokrasia bila usumbufu siku hiyo ya Jumanne.

Akiwahutubia waandishi wa habari baada ya mkutano wa usalama, Wanyanga alisema zoezi hilo litafanywa kwa kuzingatia  kanuni za kukabiliana na maradhi ya  COVID-19 bila watu  kuruhusiwa  kukusanyika wakati wa upigaji kura.

Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo,  Ali Nuno,  alionya  watakaopanga  vurugu watachukuliwa hatua za kisheria.

Wanaowania kiti hicho ni  wagombea 11, mjane wa  aliyekuwa mbunge  wa eneo  hilo,  Susan Njeri ambaye anawania kwa tikiti ya Chama cha Jubilee, George Koimburi, mgombea wa  chama cha People’s Empowerment, Anthony Kirori (Maendeleo Chap Chap), John Njoroge (Peoples Party of Kenya), Eunice Wanjiru (The New Democrats). Wagombeaji huru ni Dkt. Joseph Gichui, Zulu Thiong’o, aliyekuwa mtangazaji wa redio, James Marungo na Moses Mwenda.

  

Latest posts

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi