Ushirikiano kati ya China na Afrika unawasaidia watu wa Afrika kukabiliana na changamoto zao za kimaisha

Na Fadhili Mpunji.

Ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kwenye sekta ya ujenzi wa miundo mbinu unaendelea kuleta manufaa kwa nchi mbalimbali, na katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ushahidi na mifano mingine inaoonesha kuwa, ushirikiano huo sio tu umekuwa ni wa kunufaishana, bali pia umekuwa ni ushirikiano unaolenga moja kwa moja kutatua changamoto za watu.

Kwa watu watakaokuwa wametembelea mji wa Dar es salaam katika mwaka mmoja uliopita, watakuwa wanajua wamebahatika kuona daraja la Mfugale lililopo katika eneo la TAZARA, ambalo limeondoa kadhia ya msongamano kwa watu wanaokwenda uwanja wa ndege kutoka Posta, na wale wanaotumia barabara ya Mandela.

Hali hii pia inaonekana kwa watumiaji wa barabara ya Morogoro ambao kutokana na kuwepo kwa daraja la Kijazi, msongamano wa magari uliozoleka kwa muda mrefu sasa haupo tena.Kinachofurahiwa na wakazi wa mji wa Dar e salaam sasa kinaonekana nchini Kenya, ambako Barabara ya Nairobi Expressway iliyosubiriwa kwa muda mrefu, sasa imeanza kufanya kazi.

Also Read
Huenda mazungumzo kuhusu uchaguzi nchini Somalia yakarejelewa karibuni

Kukamilika kwa mradi huo, sio kama tu kumewashangaza wakenya wengi kutokana na kasi ya ujenzi uliokamilika ndani ya miaka miwili, bali pia kutokana na kupunguza misongamano ya magari asubuhi na jioni iliyokuwa kero kubwa kwa wakazi wa Nairobi na maeneo ya karibu.

Mwanzoni habari kubwa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo ilikuwa ni kuhusu ajira kwa wakazi wa Nairobi na wale wa maeneo ya jirani, lakini sasa kinachozungumziwa ni uzuri wa barabara, urahisi wa kusafiri na hata kupendezesha mji wa Nairobi na kuupa sura ya mji wa kisasa.

Hali hii ni sawa inayoonekana nchini Tanzania, ambako miradi ya ujenzi wa madaraja ya juu (flyovers) si kama tu inatajwa kuwa imepunguza kero ya msongamano, bali pia imeupa mji wa Dar es salaam sura mpya.

Mradi mwingine muhimu kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika utakaozinduliwa hivi karibuni, ni ule wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji cha Hujibazi, chenye uwezo wa kuzalisha kilowati elfu 15 za umeme. Hiki ni kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme wa kiasi hicho kujengwa nchini Burundi katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Also Read
Watu kadhaa wafariki Afghanistan baada ya mlipuko kutokea msikitini

Bila shaka kituo hiki hakitakuwa moja ya maeneo yanayopendezesha mji, lakini ni mradi unaotatua changamoto iliyodumu kwa zaidi ya miaka 30.Tukiichambua miradi yote hiyo tunaweza kuona ina sifa zinazofanana.

Wakati wa Nairobi wamekuwa wakihitaji barabara kama ya Nairobi Expressway kwa muda mrefu, sawa na wakazi wa Dar es salaam waliohitaji madaraja ya juu tangu enzi ya mwalimu Nyerere. Lakini mashirika ya fedha ya nchi za magharibi na makampuni ya nchi za magharibi yalipoombwa kushiriki kwenye kazi hiyo yalikataa.

Baada ya China kuwa na nguvu ya fedha na teknolojia ya ujenzi wa miundo mbinu, miradi ambayo ilitakiwa kujengwa katika miongo mitatu iliyopita katika nchi za Afrika, sasa inajengwa na kuleta unafuu kwa maisha ya watu wa nchi hizo.

Also Read
Mwanamke anayedaiwa kuiba kompyuta ya Spika Pelosi Marekani atiwa nguvuni

Ni miaka mitano sasa imefika tangu mkutano kuhusu pendekezo la Ukanda mmoja, Njia moja ufanyike hapa Beijing na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika. Mkutano ule ulifungua njia ya ujenzi wa miradi kadhaa ya miundo mbinu, baadhi ya miradi hiyo sasa inafanya kazi, na mingine inaendelea kujengwa.

Licha ya kuwa baadhi ya nchi za magharibi zimekuwa zikizungumzia vibaya pendekezo hilo kutokana na uhasama wao wa kiitikadi na China, ukweli ni kwamba utekelezaji wa miradi ya pendekezo hilo katika nchi za Afrika, umekuwa ni wa kunufaishana kati ya serikali za nchi za Afrika na makampuni ya China, na pia umesaidia kutatua changamoto zinazowagusa moja kwa moja watu wa kawaida wa nchi za Afrika.

  

Latest posts

Mataifa ya G7 kusitisha uagizaji dhahabu kutoka Urusi

Tom Mathinji

Mzozo wa Ukraine na Russia kujadiliwa katika mkutano wa G7

Tom Mathinji

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia augua Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi