Serikali ya Mynmar imewasilisha mashtaka matano mapya ya ufisadi dhidi ya kiongozi aliyeondolewa mamlakani Aung San Suu Kyi.
Afisa mmoja anasema hii inahusiana na utoaji vibali vya kukodisha na kununua ndege aina ya helikopta.
Aung San Suu Kyi, aliyezuiliwa mwezi Februari mwaka 2021 tangu kufanywa mapinduzi ya serikali, tayari anakabiliwa na mashtaka mengine matano ya ufisadi.
Kila shtaka lina hukumu ya miaka 15 gerezani ama kutozwa faini.
Suu Kyi awali alikabiliwa na mashtaka mengine na amehukimiwa kifungo cha miaka sita gerezani baada ya kuhukumiwa kwa kuagiza vifaa haramu vya mawasiliano, na kukiuka masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya Covid-19.
Wafuasi wake na makundi ya kutetea haki za binadamu wanasema kesi dhidi yake ziliwasilishwa na jeshi, ili kuhalalisha kubanduliwa kwake mamlakani na kumzuia kurejea kwenye ulingo wa siasa.
Jeshi limekanusha shtuma dhidi yake kuhusiana na hukumu hizo.