Utawala wa Taliban washtumiwa kwa utumuzi wa nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji

Umoja wa Mataifa umelaani  kundi la Taliban kwa kile ulichokiita mwendendo  unaozidi  wa  kutumia   mabavu dhidi ya  wapinzani, wiki chache baada ya kundi  hilo kutwaa uongozo nchini Afghanistan.

Umoja huo  ulisema wapiganaji wa Taliban waliwaua watu wanne wakati wa maandamano ya hivi karibuni. Maandamano yamefanyika kote Afghanistan tangu kutekwa kwa mji mkuu Kabul mnamo  tarehe 15 Agosti,  huku waandamanaji wakitaka  kuheshimiwa kwa haki za wanawake na uhuru zaidi.

Also Read
Baadhi ya Maseneta Marekani wadinda kuidhinisha ushindi wa Biden

“Tunaagiza kundi la Taliban kusitisha mara moja utumizi wa nguvu kupita kiasi na kuwazuilia wanaotekeleza haki zao kupitia maandamano ya amani pamoja na wanahabari wanaokusanya habari kuhusu maandamano hayo,” ulisema umoja wa Mataifa.

Also Read
Maafisa wa usalama nchini Uganda washtumiwa kwa kuwajeruhi wanahabari waliokuwa wakiripoti kumhusu Bobi Wine

Wapiganaji wa Taliban walivamia Afghanistan mnamo mwezi Agosti,  huku wakiteka vituo vya mikoa na mwishowe mji mkuu wa Kabul  chini ya muda wa wiki mbili.

Also Read
Mifumo hafifu ya sheria yalaumiwa kwa ongezeko la dhuluma za kimapenzi kwa watoto

Marekani  iliongoza shughuli ya uwokoaji   ya kusafirisha  watu kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Kabul na  ikahamisha zaidi ya watu  alfu 120 kabla ya kuondoa  vikosi vyake mnamo 31 Agosti.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi