Utawala wa Taliban watakiwa kubuni serikali inayowajumuisha wote

Russia, China, Pakistan na Marekani zinashirikiana katika kuhakikisha watawala wapya nchini Afghanistan wa Taliban wanatimiza ahadi zao hasa katika kubuni serikali inayowawakilisha wote na kuzuia kusambaa kwa ghasia.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Russia, Sergey Lavrov,amesema nchi hizo nne zinawasiliana.

Also Read
Washukiwa wa mauaji ya watu wanne Kisii kuzuiliwa kwa siku 10 zaidi

Alisema wawakilishi kutoka Russia, China, na Pakistan hivi majuzi walisafiri kwenda Qatar na hadi mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, kwa mashauriano na wataliban na wawakilishi aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hamid Karzai na Abdullah Abdullah, aliyeongoza baraza la mashauriano la serikali iliyopinduliwa na wataliban.

Also Read
Balozi wa Pakistan Saqlain Syedah apongeza ushirikiano kati ya Kenya na Pakistan

Wataliban wameahidi kubuni serikali inayowawakilisha wote na kuheshimu haki za wanawake.

Lakini hatua za hivi majuzi zinaonyesha kwamba wataliban huenda wanarejelea utawala wa kukandamiza hata zaidi hasa kwa wanawake na wasichana.

Tangu kuchukua hatamu kutoka kwa serikali iliyoungwa mkono na serikali, Utawala wa Taliban umewakubalia tu wavulana na walimu wa kiume kurejea shuleni huku wale wa kike wakirejea kwa awamu.

Also Read
Watu wanane zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Kulingana na ripoti ya Umoja wa mataifa, wanafunzi milioniĀ  4.2 hawajajiunga na shule nchini Afghanistan, ambapo asilimia 60 kati yao ni wasichana.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi