Uwanja wa Bin Ali utakaondaa kipute cha kombe la dunia mwaka 2022 wazinduliwa

Uwanja wa Ahmad Bin Ali ulizinduliwa rasmi  Ijumaa nchini Qatar  sherehe hiyo pia ikiadhimisha miaka 2 kabla ya mechi  ya fainali kuwania kombe la dunia mwaka 2022  kuchezwa.

Uzinduzi wa uwanja huo unaomudu mashabiki 40,000 uliambatana na sherehe za kitaifa nchini Qatar huku ukiwa wa hivi punde  na wa nne kuwa tayari kwa  kindumbwendumbwe cha kombe la dunia baada ya ya   Khalifa International, Al Janoub na  Education City .

Also Read
Timu ya Olunga Duhail yaangukia Ahly Droo ya kombe la dunia kwa vilabu mwezi ujao
Also Read
Madereva wasubiri kwa ghamu mashindano ya dunia ya Kenya

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Rais wa FIFA  Gianni Infantino, Rais wa shirikisho la soka barani Asia  Shaikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa, kinara wa CONMEBOL Alejandro Domínguez na mwenzake wa  UEFA Aleksander Čeferin.

Also Read
Daniel Wanjiru apigwa marufuku ya miaka 4 kwa ulaji muku

Dimba la kombe la dunia litaandaliwa  kati ya Novemba 18 na Disemba 18 mwaka 2022.

  
  

Latest posts

Hassan Wario alipa shilingi milioni 3.6 na kuepuka kifungo cha miezi sita gerezani

Tom Mathinji

Malkia Strikers yafunga mechi za makundi kwa kuilaza Burundi seti 3-0 mashindano ya kuwania kombe la Afrika

Dismas Otuke

Waziri wa zamani wa michezo Hassan Wario afungwa miaka 6 gerezani na kulipa faini ya shilingi milioni 3 nukta 6

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi