Uzinduzi wa albamu ya Mbosso waahirishwa

Tangazo hili limetolewa muda mfupi uliopita na msanii huyo Mbosso kupitia akaunti yake ya Instagram.

Uzinduzi huo wa albamu kwa jina “Definition of Love” ulikuwa umepangiwa kufanyika kesho tarehe 20 mwezi Machi mwaka huu wa 2021.

Usimamizi wa WCB kampuni ambayo inamsimamia Mbosso ulikuwa awali umepanga kwamba hafla ianze saa moja jioni katika eneo la mlimani City Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania lakini nchi hiyo kwa sasa inaomboleza kifo cha Rais Magufuli.

Also Read
Zuchu afurahia kukutana na babake mzazi

Wasanii wengi nchini Tanzania wameguswa na msiba huo kwa sababu marehemu Magufuli alikuwa amewatambua sana na kuwezesha kuendelea kwa sanaa yao.

Usimamizi wa WCB haujatoa tarehe mbadala ya kuzindua kazi ya Mbosso na labda itatangazwa baada ya mazishi ya Rais Magufuli ambayo yatafanyika Alhamisi tarehe 25 mwezi huu wa Machi mwaka 2021.

Also Read
Mwanamuziki wa Tanzania CPwaa aaga Dunia

Albamu ya Mbosso Definition of Love ina vibao 12 ambavyo ni; Mtaalam, Kiss Me, Baikoko ambao amemhusisha Diamond Platnumz na Tulizana ambao aliimba na Njenje wa bendi ya Kilimanjaro.

Wimbo wa tano kwenye albamu hiyo unaitwa Yalah, wa sita Sakata ambao aliimba na Flavour, wa saba Pakua aliouimba na Rayvanny ambaye pia ni wa kundi la WCB na wa nane ni Karibu ambao aliimba tena na Diamond.

Also Read
Albamu Ya Mr. Seed

Nyimbo nyingine ni Your Love ambao aliimba na Liya, Kadada alouimba na Darassa, Yes wake na Spice Diana na Nipo Nae ambao ameimba peke yake.

Aliongezea nyimbo nyingine mbili ambazo anarejelea kama “Bonus Tracks” mmoja unaitwa Limevuja na mwingine Kamseleleko ambao alimshirikisha Baba Levo.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi