Victor Wanyama astaafu soka ya kimataifa

Victor Wanyama ametangaza kustaafu rasmi kutoka soka ya kimataifa baada ya kucheza jumla ya mechi 64 na kufunga magoli 7 akivalia sare ya Harambee Stars.

Wanyama ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Montreal Impact katika ligi kuu ya Marekani MLS amewapongeza mashabiki waliomuunga mkono akiwa katika Harambee Stars kwa miaka 14 iliyopita akicheza mchuano wa kwanza dhidi ya Nigeria mwaka 2007  na pia kuwa nahodha wa timu hiyo kwenye fainali za AFCON mwaka 2019 nchini Misri.

Also Read
Kenya yaibwaga Ethiopia Cecafa

Wanyama alitemwa kutoka timu ya taifa ya Kenya punde baada ya mechi za kufuzu kombe la Afrika mwezi Machi mwaka huu kwa njia ya kutatanisha  huku Michael Olunga akipokezwa unahodha na kocha wa wakati huo Jacob Mulee , na huenda iwe ndio sababu iliyochangia kuchukua hatua hiyo ya mapema.

Also Read
Yanga yamnyatia kocha Auseems wa Leopards

Kiungo  huyo wa zamani wa Tottenham ,aliitwa kupigia Harambee Stars kwa mara ya kwanza Mei mwaka 2007,  akiwa na umri wa miaka 15 katika mchuano wa kirafiki dhidi ya Nigeria na alicheza mechi zote 6 za Kenya ,kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2010 .

Also Read
Somalia yahimiza Kenya kufungua ubalozi wake nchini humo

Mugubi Wanyama amekuwa  nahodha wa Harambee Stars tangu mwaka 2013 na alicheza mchuano wa mwisho Novemba mwaka uliopita waliposhindwa mabao1-2  na Comoros ugenini katika pambano la kufuzu kwa dimba la Afcon.

Kwenye waraka wake ,Wanyama amesema ataendelea kuwapa Support wachezaji wa Harambee Stars na kuahidi pia kushirikiana na FKF siku zijazo .

 

 

  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi