Vihiga Queens Fc walenga kuanza vyema ligi ya mabingwa

Waakilishi wa ukanda wa Afrika mashariki kwenye makala ya kwanza ya kipute cha kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika mwaka huu , Vihiga Queens Fc watalenga kuandikisha historia , watakposhuka uwanjani Jumamosi jioni kwa pambano la kwanza la kundi B dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Vipusa hao wanaofadhiliwa na kaunti ya Vihiga walijikatia tiketi kushiriki mashindano hayo baada ya kunyakua kombe la CECAFA waliopoishnda Central Bank of Ethiopia mabao 2-1 katika fainali.

Also Read
Serikali za kaunti zatakiwa kusaidia katika vita dhidi ya minyoo shuleni
Vihiga Queens wakiwa  mazoezini katika uwanja wa June 30th Cairo

Queens waliwasili Cairo mapema juma hili na wamekuwa wakipiga zoezi katika uchanjaa wa June 30 kujiandaa kwa mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mamelodi Jumamosi jioni.

Also Read
Kenenisa Bekele ajiondoa London Marathon kutokana na Jeraha

Itakuwa ni mechi ngumu kwa waakilishi wa Kenya kutokana na ubora wa Mamelodi Sundowns.

Queens watakuwaw wakitegemea pakubwa huduma za mshambulizi bora wa CECAFA Jentrix Shikangwa .

Timu 8 kutoka kanda zote za Afrika zitashiriki mashindano hayo yatakayoanza rasmi Ijumaa Novemba 5 kwa mechi kati ya wenyeji WadI Degla na AS Mande kutoka Mali katika kundi A kuanzia saa kumi alasiri ,kabla ya Malabo King Fc kutoka Equitorial Guinea kupimana nguvu na Hasaacas ladies Fc ya Ghana saa moja usiku.

Also Read
Jumuiya ya Ulaya yapunguza uagizaji mafuta kutoka Urusi

Mechi zote za patashika hiyo zitapeperushwa mbashara na runinga ya KBC Channel 1 na Y254.

  

Latest posts

Kocha wa Gor Mahia Andreas Spier afunganya virago

DOtuke

PSG yamfurusha Pochettino baada ya kuwa usukani kwa miezi 18

DOtuke

Timu ya taifa ya raga yanoa makali kabla ya michuano ya Jumuiya ya Madola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi