Vihiga Queens watawala historia ya soka ya Kenya mwaka 2021

Historia kubwa iliyosimama mwaka 2021 katika soka ni hatua ya klabu ya Vihiga Queens kushiriki makala ya kwanza ya mashindano ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake,baada ya kutwaa kombe la Cecafa jijini Nairobi walipowaadhibu Commercial Bank of Ethiopia mabao 2-1 katika fainali.

Queens walipoteza mechi mbili na kushinda ,moja katika kundi B ,wakipigwa moja bila na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,kabla ya kuilemea ASFAR ya Moroko mabao 2-0 na kuchakazwa mabaao 4-0 na River Angels kutoka Nigeria .

Katika soka ya wanaume Gor Mahia walishibndwa kufuzu kwa awamu ya makundi ya kombe la shirikisho la soka Afrika kwa mwaka wa tatu mtawalia ,wakati mabingwa wa ligi ya Kenya Tusker FC pia wakitimuliwa katika mataji yote ,ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho ,wakirejea katika soka ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne.

Also Read
Kenya yatemwa nje na CAF kushiriki mechi za kufuzu kombe la AFCON mwaka ujao

K’Ogalo walainza vyema katika mchujo wa pili wa kombe la shirikisho wakiilaza Al Ahly Merowe ya Sudan 3-1 ,lakini wageni hao wa Sudan wakakosa kusafiri kuja Kenya kwa mechi ya marudio .

Gor Mahia wakipambana na Otoho uwanjani Nyayo

Safari ya Gor ilitamatishwa na klabu ya AS Otoho d’Oyo ya Congo Bazzavile baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 .

Tusker walinyakua ubingwa ligi kuu na kupata tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa Afrika wakianza kwa makeke na kuititiga Arta Solar 7 ya Djibouti mabao 4-1 lakini wakakiona cha mtema kuni waliponyukwa jumla ya magoli 5-1 na miamba wa Misri Zamalek katika mchujo wa pili .

Also Read
Afrika kusini yanakili kisa cha pili cha Monkeypox

Wagema mvinyo Tusker walishuka kucheza kombe la shirikisho ambapo pia walitimuliwa na klabu ya CS Sfaxien kutoka Tunisia bao 1-0.


Mwaka huu pia haukuwa mzuri kwa timu ya taifa Harambee Stars iliyokosa kufuzu kwa raundi ya tatu nay a mwisho kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar.

Kenya iliyokuwa na mabadiliko matatu ya wakufunzi katika mechi 6 za kundi F kufuzu kwa kombe la dunia ilianza kwa kupiga sare nyumbani dhidi ya Uganda ,kabla ya kupiga sare ugenini dhidi ya Rwanda na kupoteza mabao 5-0 dhidi ya Mali ugenini nchini Moroko.

Katika mkwangurano wan ne , Kenya iliambulia kichapo bao 1-0 nyumbani dhidi ya Mali na kutoka sare ya 1-1 jijini Kampala dhidi ya Uganda Cranes kabla ya kuandikisha ushindi wa kwanza na wa pekee ,mabaoa 2-1 nyumbani dhidi ya Rwanda.

Also Read
China yawalenga wanafunzi katika kudhibiti Covid-19
Kenya wakicheza dhidi ya Rwabda uga wa Nyayo

Mali waliongoza kundi hilo kwa pointi 16,wakijivunia kutopoteza mechi ,wakifuatwa na Uganda kwa alama 9 ,tatu zaidi ya Kenya.

Harambee Stars ilishuhudia mageuzi matatu ya kocha mkuu akipigwa kalamu Francis Kimanzi na Jacob Ghost Mulee kupewa jukumu hilo na kutimuliwa mwaka mmoja baade huku Engin Firat,akisha hatamu k,japo kwa mechi nne tu.

Hata hivyo muuhula wa pili wa utawala wake Nick Mwendwa katika FKF ulifikia tamati ghafla bin vuu baada ya waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed kuvunjilia mbali shirikisho na kubuni kamati ya ya muda .

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Tume ya EACC yachunguza wizi wa shilingi milioni 72 za kaunti ya Siaya

Dismas Otuke

Watu 171 wafariki kwenye mkanyagano wakati wa mechi ya soka nchini Indonesia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi