Vikosi vya Tigray vyalaumiwa kwa ukiukaji wa haki za Kibinadamu

Kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema vikosi vya Tigray vimewauwa mamia ya raia kwenye uhalifu wa kivita katika miji miwili ambayo kundi hilo linamiliki katika eneo la Amhara.

Kulingana na kundi hilo Mauaji hayo yalitekelezwa kati ya tarehe 31 mwezi Agosti na tarehe 9 mwezi Septemba mwaka 2021, kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo.

Also Read
Maafisa wa usalama waliwaua raia 75 nchini Ethiopia katikati ya mwaka jana

Walioshuhudia walielezea tume hiyo ya haki za binadamu kwamba waliona wapiganaji wa Tigray huko Chenna na Kobo wakiwauwa jumla ya raia 49 katika visa tofauti.

Also Read
Kamanda wa LRA nchini Uganda ataka kesi dhidi yake ihamishiwe ICC

Mkurugenzi wa usuluhishaji mizozo wa shirika la Human Rights Watch, Lama Fakih, alisema vikosi vya Tigray, vilionyesha ukatili kwa maisha ya mwanadamu na sheria kuhusu vita kwa kuwauwa watu waliokuwa wakizuiliwa.

Also Read
UNHCR yahofia usalama wa raia kaskazini mwa Msumbiji

Vikosi vya Tigray havijajibu madai hayo. Shirika la Human Rights Watch lilihimiza umoja wa mataifa kuanzisha uchunguzi wa kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita na ukiukaji haki za binadamu kwa pande zote kwenye mzozo wa Tigray.

  

Latest posts

Mwanaume mmoja ashtakiwa kwa makosa saba ya mauaji Marekani

Tom Mathinji

Uganda yaidhinisha Kiswahili kuwa Lugha rasmi

Tom Mathinji

Walinda usalama wawili wa Umoja wa Mataifa wauawa nchini Mali

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi