Vinka atetea kitendo chake

Mwanamuziki wa Uganda Veronica Luggya maarufu kama Vinka ametetea hatua yake ya kumpiga mtu aliyeshika sehemu zake za siri akiwa jukwaani Jijini Juba, nchini Sudan Kusini.

Akizungumza kwenye mahojiano na wanahabari wa kituo kipya cha redio cha mitandaoni huko Uganda, Vinka alisema hatua aliyochukua ndiyo ilikuwa mwafaka kwa wakati huo akisema mtu huyo alimdhulumu kimapenzi na kamwe hakubali tabia kama hizo.

Also Read
Rayvanny atangaza jina la kampuni yake ya muziki

Mtangazaji mmoja wa kituo hicho cha redio ambacho kilikuwa kinazinduliwa rasmi anaonelea kwamba jamaa huyo angekamatwa na kushtakiwa.

Video ya tukio hilo linalohusisha Vinka wa kampuni ya muziki ya Sony ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakiunga mkono hatua aliyochukua.

Also Read
Mkalimani ajitetea!!

Tamasha hilo la Sudan Kusini ndilo la kwanza kubwa ambalo mwanamuziki Vinka amehudhuria tangu kujifungua.

Hata hivyo wapo wanaoshikilia maoni tofauti na ya wanaomuunga mkono Vinka.

Mwanamuziki mwenzake kwa jina Khalifa Aganaga anashtumu kitendo cha Vinka cha kumzaba makofi jamaa aliyemshika visivyo. Anasema jamaa huyo alikuwa tu anajifurahisha na kwamba Vinka alijisababishia yaliyomfika.

Also Read
Bobi Wine akamatwa punde baada ya kuidhinishwa kuwania Urais nchini Uganda

Kulingana naye, Vinka angevaa mavazi ya heshima hangekumbana na tatizo hilo.

Vinka hajasema lolote kuhusu maoni ya Khalifa Aganaga.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi