Viola Davis aandikisha historia!

Viola Davis muigizaji wa Marekani kwenye filamu za Hollywood ameandikisha historia ya kuwa muigizaji wa kike wa asili ya Afrika au ukipenda mmarekani mweusi aliyeteuliwa mara nyingi kuwania tuzo za Oscar.

Uteuzi wa maajuzi kutokana na jukumu lake kwenye filamu ya “Ma Rainey’s Black Bottom” umevunja rekodi ambayo alikuwa anashikilia kwa pamoja na Octavia Spencer ambaye ameteuliwa mara tatu kuwania tuzo za Oscar na akashinda moja.

Kulingana na matangazo ya jumatatu ya walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar awamu ya 93, Viola ameteuliwa kuwania tuzo la muigizaji mkuu bora wa kike.

Also Read
ICM yalaumiwa kwa ubaguzi

Viola Davis ameteuliwa mara nne kuwania tuzo za Oscar na alishinda tuzo la muigizaji msaidizi bora wa kike kutokana na jukumu lake kwenye filamu iitwayo “Fences” mwaka 2017.

Davis aliwahi kuteuliwa kuwania tuzo la muigizaji bora msaidizi wa kike kutokana na filamu ya “Doubt,” akateuliwa kuwania tuzo la muigizaji bora kutokana na jukumu lake kwenye filamu “The Help” na akateuliwa kuwania tuzo la muigizaji msaidizi bora wa kike kwenye filamu “Fences” ambalo alishinda.

Wanawake weusi nchini Marekani wamekuwa wakiandikisha historia katika ulingo wa burudani na wa hivi karibuni zaidi ni mwanamuziki Beyonce.

Also Read
Mazishi ya Cicely Tyson kuandaliwa leo

Katika tuzo zilizofanyika jumapili za Grammy, ilibainika kwamba Beyonce ameshinda tuzo 28 za Grammy kufikia sasa.

Mwingine ni mchekeshaji Tiffany Haddish ambaye alishinda tuzo la Grammy katika kitengo cha albamu bora ya uchekeshaji kutokana na kazi yake inayofahamika kama, “Black Mitzvah”.

Mwanadada huyo ambaye alijuzwa kuhusu ushindi wake akiendeleza kazi nyingine ya kuunda kipindi cha watoto, alidodonkwa na machozi ya furaha akisema mwanamke mweusi hajashinda katika kitengo hicho tangu mwaka 1986.

Viola Davis anashindana na Andra Day kutokana na jukumu lake kwenye filamu ya “The United States vs. Billie Holiday”, Vanessa Kirby wa filamu ya “Pieces of a Woman”, Frances McDormand wa filamu iitwayo “Nomadland” na Carey Mulligan wa filamu inayojulikana kama “Promising Young Woman”.

Filamu yao ya “Ma Rainey’s Black Bottom” inawania tuzo tano kwenye awamu ya 93 ya tuzo za Oscar na washindi watatangazwa na kutuzwa tarehe 26 mwezi Aprili mwaka huu wa 2021.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi