Viongozi wa kaunti ya Mombasa waelezea wasiwasi kuhusu kutoweka kwa watu

Wabunge wawili wa kaunti ya mombasa wamesema watawasilisha bungeni mswada wa pamoja kuwataka waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i,inspekta Generali wa polisi Hilary Mutyambai na mkuu wa idara ya upelelezo George Kinoti, kuhojiwa kuhusu kutoweka kwa watu.

Mbunge wa mvita Abdulswamad Nassir na Seneta wa Mombasa Mohamed Faki, wanataka kamati ya pamoja ya mabunge ya seneti na bunge la kitaifa kueleza kuhusu kutoweka kwa Prof. Abdiwahab Sheikh Abdusamad na kupatikana kwa miili iliyo kuwa na majeraha mengi katika mto Tana.

Also Read
Serikali yatakiwa kuhusisha wadau wote katika oparesheni ya Kapedo

Prof. Abdusamad, anasemekana kutekwa nyara na watu wasiojulikana  kwenye barabara ya Turbman iliyo karibu na City Market na kuingizwa kwenye gari moja lilillokuwa likisubiri. Juhudi za kumtafuta hazijafalu.

Also Read
Waziri Matiang'i kuhojiwa na bunge kuhusu usalama wa Naibu Rais William Ruto

“Tumeghadhabishwa na hatua hizo, tutashirikiana katika shughuli hii kwa kuwa lazima mtu awajibike kutokana na matendo hayo. Tutawasilisha hoja ya pamoja wiki hii kuwataka maafisa hao wakuu serikalini kuelezea mbona maovu haya yanatendeka,” alisema Nassir.

Also Read
Wazee wa Kaya wataka mahakama ya kitamaduni ya Mijikenda itambuliwe kisheria

Familia ya Profesa Abdiwahab inataka kufahamishwa aliko baada ya kutekwa nyara katikati mwa Jiji la Nairobi.

Mohamed Huri Ibrahim, ambaye ni mwenyekiti wa jamii ya wasomali Jijini Mombasa, alisema visa vya watu kutoweka ni vya kusikitisha na vinapaswa kukomeshwa.

  

Latest posts

Aliyekuwa mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ajitosa katika ulingo wa siasa

Tom Mathinji

#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

John Madanji

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi