Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Murang’a wanataka aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth kuwa mgombea mweza wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wakiongea katika kanisa la AIPCA Kihoya eneo la  Kangema wakati wa ibada ya jumapili, viongozi hao walisema rekodi ya maendeleo ya Kenneth inafahamika vyema na anafaa kuhudumu kwenye wadhifa wa naibu rais.

Also Read
Maambukizi ya Covid-19 yanapenyenza katika kaunti zilizo nje ya zile zilizofungwa

Wabunge hao Mary Waithera wa Maragua,Joseph Nduati wa Gatanga, Peter Kimari wa Mathioya na Ruth Wangari wa Kigumo walisema kuwa kaunti ya Muranga imekuwa ikitekeleza wajibu muhimu katika siasa za taifa hili wakiongeza kuwa wakadi umewadia kwa Kenneth kuhudumu katika wadhifa huo.

Waithera alisema Kaunti ya Murang’a iliunga mkono kikamilifu kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta katika awamu ya kwanza na ya pili huku akisema kuwa hawatachagua wadhifa mwingine isipokuwa ule wa naibu rais.

Also Read
Zoezi la kukusanya saini milioni 4 kwa ajili ya BBI kuzinduliwa Jumatano

“Tunataka mwana wetu Kenneth kufikiriwa wadhifa wa naibu rais katika mkataba wa handshake. Na sisi watu wa Murang’a tunamuunga mkono,” alisema Waithera.

Also Read
Uhuru: Niko tayari kuitumikia nchi tena baada ya kustaafu

Kwa upande wake, Peter Kenneth aliahidi kuwahudumia vilivyo watu wa eneo la mlima Kenya iwapo atapewa wadhifa wa naibu Rais.

“Iwapo nitapata wadhifa wowote katika serikali, sitawaaibisha watu wa kanda hii,” aliahidi Kenneth.
Aliwaonya wakazi wa mlima kenya dhidi ya kuhadaiwa na viongozi ambao watasababisha chuki na machafuko.

  

Latest posts

Watu 19 wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni Kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Watu wawili zaidi wametolewa katika migodi ya Abimbo

Tom Mathinji

Kliniki mpya ya ugonjwa wa saratani yafunguliwa katika kaunti ya Nandi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi