Viongozi wa Kilifi waibua wasi wasi kutokana na ongezeko la visa vya COVID-19

Baadhi ya viongozi katika Kaunti ya Kilifi wameelezea hisia zao kuhusiana na ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19.

Wakiongozwa na Katibu Mwandamizi katika Wizara ya Ugatuzi Gideon Mung’aro na Naibu Gavana wa Kaunti ya Kilifi Gideon Saburi, viongozi hao waliwahimiza wakazi kuzingatia ipasavyo maagizo ya Wizara ya Afya ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
William Ruto amtakia Raila Odinga afueni ya haraka

Akiongea wakati wa mazishi ya watoto wawili wa Kasisi Tom Dawa wa Kanisa la Kianglikana sehemu ya Thalathamel huko Malindi, Mung’aro alisema kuna haja ya kuzingatia vilivyo maagizo hayo.

Also Read
Visa vya Covid-19 vyaripotiwa katika shule 7 kaunti ya Narok

Saburi aliongeza kuwa watu wanapaswa kufahamu kuwa ugonjwa wa COVID-19 upo na hawapaswi kupotoshana kuwa haupo.

Saburi, ambaye aliwahi kuambukizwa ugonjwa huo, alisema kuwa sasa amekuwa mwanaharakati wa kukabiliana na janga hilo.

Kaunti ya Kilifi imekuwa ikishuhudia ongezeko kubwa la visa vya maambukizi ya virusi vya Korona katika siku za hivi majuzi.

Also Read
Chuo cha sayansi na teknolojia cha Rift Valley kufungua milango yake kwa wanafunzi

Mnamo tarehe 16 mwezi huu, kaunti hiyo ndiyo iliyonakili visa vingi zaidi humu nchini siku hiyo ambapo watu 224 walithibitishwa kuambukizwa.

  

Latest posts

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Watu wawili wafariki baada ya mashua kuzama Homa Bay

Tom Mathinji

Bunge lachunguza nyongeza ya bei za mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi