Viongozi wa Magharibi wakutana na Rais Kenyatta Katika Ikulu ya Nairobi

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na baadhi ya viongozi wa eneo la Magharibi ya Kenya waliomtembelea katika ikulu ya Nairobi.

Rais Kenyatta amewahakikishia viongozi hao kutoka kaunti tano za Kakamega, Bungoma, Busia, Trans-Nzoia na Vihiga, kuwa serikali imejitolea kuhakikisha miradi inayoendelea ya maendeleo katika eneo hilo inakamilishwa.

Also Read
Ben Pol azungumzia talaka kwa mara ya kwanza

Kwa upande wao, viongozi hao waliojumuisha waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa na magavana Wycliffe Oparanya wa Kakamega, Wycliffe Wangamati wa Bungoma, Wilbur Ottichillo wa Vihiga na Sospeter Ojaamong wa Busia, walimshukuru Rais kwa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo walisema imeboresha maisha ya watu wa eneo la Magharibi ya nchi.

Also Read
Museveni aapishwa kuhudumu kama Rais wa Uganda kwa kipindi cha sita
Viongozi wa Magharibi mwa nchi Katika Ikulu ya Rais Jijini Nairobi.

Viongozi hao hasa walimshukuru Rais Kenyatta kwa kuchukua hatua iliyowezesha kubatilishwa kwa hatua ya kuchapisha milima ya Chetambe kwenye gazeti rasmi la serikali kama hifadhi ya msitu wa kitaifa.

Also Read
Uhuru Kenyatta: UNCTAD inauwezo wa kukwamua uchumi wa ulimwengu

Kuchapishwa kwa msitu huo wenye ardhi ya ekari 406 kwenye gazeti rasmi la serikali mwezi Julai mwaka 2021, kungesababisha zaidi ya watu 10,000 kuachwa bila makazi katika wadi za Maraka na Mihuu katika eneo bunge la Webuye Mashariki kaunti ya Bungoma .

  

Latest posts

Atlas Lions ya Moroko yaiparuza Ubelgiji Kombe la Dunia

Dismas Otuke

Rais Ruto: Kenya ina uwezo wa kujiendeleza kiuchumi

Tom Mathinji

Visa 36 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi