Viongozi wa Migori waagizwa kuhamasisha wanafunzi wote kurejea shuleni

Kamishna wa Kaunti ya Migori Boaz Cherutich amewaagiza Machifu wote na manaibu wao kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa kurejea shuleni.

Agizo hili linajiri kufuatia ripoti kwamba wasichana kadhaa wa shule huenda wasirejee shuleni mwezi huu, baada ya kutungwa mimba wakati wa likizo ndefu nyumbani kutokana na janga la virusi vya korona.

Also Read
Shirika la KTDA lataka maafisa wake wanne wanaozuiliwa kuachiliwa huru

Akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa ushauri kuhusu mimba za mapema ulioandaliwa na shirika lisilo la serikali la Triggerise, Cherutich amesikitishwa na kiwango kikubwa cha mimba za mapema miongoni mwa wasichana wa sehemu hiyo.

Mbali na kutilia maanani kukita maadili miongoni mwa vijana kupitia maafisa wa utawala wa sehemu hiyo, serikali ya kitaifa na ile ya kaunti katika sehemu hiyo zitahakikisha kwamba lile linalohitajika litafanywa, kuhakikisha wasichana wanadumu madarasani kama vile kuwapa visodo kila mara.

Also Read
DCI yawaonya wanawake dhidi ya walaghai mitandaoni

“Tutafanya kila tuwezalo pamoja ili kukabiliana na kasi ya kutungwa mimba kwa wasichana katika eneo hili, jambo linaloathiri elimu na afya yao,” akasema.

Also Read
Marekani kuisaidia kaunti ya Mombasa kuboresha utoaji wa huduma

Cherutich amesema shirika jipya la Triggerise, ambalo linakabiliana na mimba za mapema miongoni mwa wasichana katika sehemu hiyo, limewasili wakati ufaao kuunga mkono vita dhidi ya mimba za mapema katika sehemu hiyo.

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi