Viongozi waliokuwa afisini wahifadhi viti vyao uchaguzi wa NOCK

Viongozi wote ambao wamekuwa wakihudumu afisi  muhula uliokamilika ,wamehifadhi nyadfa zao kwenye uchaguzi wa  kamati  ya  Olimpiki nchini NOCK ullioandaliwa  Alhamisi jijini Nairobi.

Wagombezi waliokuwa wanawania kwa mara ya kwanza walipoteza takriban wote  isipokuwa Barnaba Korir aliyechaguliwa mwanachama wa kamati kuu.

Francis Mutuku alichaguliwa katibu mkuu ,kwa kupata kura 18 dhidi ya 2 za Francis Kinyili Paul maarufu  kama FK Paul ambaye alikuwa katibu mkuu katika afisi iliyopita akisaidiwa na Mutuku huku Andrew Mudibo akizoa kura 5.

Also Read
Bright Starlets waimarisha mazoezi kukabiliana na vidosho wa Kenya
Barnaba Korir achaguliwa mwanachama wa kamati kuu

Katika wadhfa wa mtunza hazina,Anthony Kariuki alihifadhi kwa kupata kura 20 dhidi ya 7 za Moses Mbuthia.

Paul Tergat  alichaguliwa bila kupingwa sawa na waakilishi wa wanamichezo Hellen Obiri na Humprey .

Paul Tergat achaguliwa bila kupingwa kuhudumu kwa muhula wa pili kuwa Rais
Humprey Khayange mwakilishi wa wanaridha 

Shadrack Maluki alihifadhi  kiti cha naibu rais wa kwanza  akipata  kura 18  dhidi ya John Kilonzo na  Nahashon Randiek walipata kura 5 na 4 mtawalia wakati Waithaka Kioni pia akishinda kiti cha naibu rais wa pili kwa  kura 22 dhidi ya 5 zake Tegla Lorupe.

Also Read
Engin apewa mkataba wa miezi miwili kuifunza Harambee Stars
Hellen Obiri achaguliwa mwakilishi wa wanariadha

Paul Otula, Barnaba Korir na Winnie Kamau  walichaguliwa wanachama wa bara kuu la NOCK kwa kuzoa kura 22,16 na 14 mtawalia.

Matokeo kamili ya uchaguzi wa NOCK

President

Paul Tergat (bila kupingwa)

First Deputy President

Shadrack Maluki (18)

John Kilonzo (5)

Nashon Randiekn (4)

Second Deputy President

Waithaka Kioni (22)

Tegla Loroupe (5)

Secretary General

Francis Mutuku (18)

Andrew Mudibo (5)

Francis Paul (2)

Deputy Secretary General

Mohamed Shoaib (18)

Also Read
Kenya Morans waanza FIBA Afrobasket kwa kichapo cha 70-88 na Ivory Coast

James Chacha (1)

Francis Karugu (8)

Treasurer

Anthony Kariuki (20)

Moses Mbuthia (7)

Deputy Treasurer

John Ogolla (22)

Agnes Oluoch (5)

Executive Committee member

Paul Otula (22)

Barnaba Korir (16)

Winnie Kamau (14)

Benjamin Musa (10)

Charles Mose (7)

Suleiman Sumba (6)

June Waweru (5)

Women Representative

Paurvi Rawal (14)

Mududa Waweru (11)

Athlete Representatives-Male

Humphrey Kayange (Bila kupingwa)

Athlete Representatives-Female

Hellen Obiri (Bila kupingwa)

Maafisa waliochaguliwa  watahudumu  kwa miaka minne ijayo.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi