Visa 193 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Taifa hili limenakili visa  193 vipya vya Covid-19 kutoka kwa sampuli 5,207 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini sasa kimefikia asilimia 3.7.

kati ya visa hivyo,161 ni raia  wa kenya ilhali 32 ni raia wa kigeni. Watu 109  ni wa kiume na 84 ni wa kike. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi minne na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 92.

Also Read
Watu 310 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Jumla ya visa 321,111 vya maambukizi vimethibitishwa.

Wagonjwa 1,018 zaidi wamepona ugonjwa huo, 924 kutoka utunzi wa nyumbani na 94 kutoka hospitali mbali mbali kote nchini.

Jumla ya wagonjwa 294,035 wamepona Covid-19 hapa nchini.

Also Read
Benki ya KCB ‘kuwaajiri’ wanafunzi 50 bora wa KCSE kabla kujiunga na vyuo vikuu

Wagonjwa 11 zaidi wameaga dunia kulingana na takwimu kutoka hospitali mbali mbali kati ya mwezi Disemba mwaka 2021 na mwezi Januari mwaka 2022.

Hii imeongeza idadi ya wagonjwa ambao wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia 5,578.

Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 548 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini, huku 4,950 wakitibiwa wakiwa nyumbani.

Also Read
Serikali kutambua wauguzi kupitia tuzo za Beyond Zero Health Awards

Wagonjwa 20 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, huku wote wakitumia mitambo ya kuwasaidia kupumua.

Hadi kufikia tarehe 27 mwezi Januari mwaka 2022, jumla ya watu 11,858,965 walikuwa wamechanjwa Covid-19 kote nchini. Kati ya Idadi hiyo watu 6,395,879 wamechanjwa awamu ya kwanza na 5,291,450 wamechanjwa kikamilifu.

  

Latest posts

Wanamichezo 11 wapokea msaada wa masomo kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini NOCK

Dismas Otuke

Watu wawili wafariki baada ya jengo kuporomoka Kiambu

Tom Mathinji

TIFA: Uwaniaji Urais wa Raila-Karua ni maarufu zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi