Visa 230 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Watu 230 zaidi hapa nchini wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 6,515 katika muda wa saa 24.

Idadi jumla ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona hapa nchini sasa ni 98,184.

Kupitia kwa taarifa, wizara ya afya ilisema kati ya visa hiyo 230 vipya vilivyonakiliwa, 221 ni wa Kenya ilhali 9 ni raia wa kigeni.

Also Read
Visa 646 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Waathiriwa 152 ni wa kiume na 78 ni wa kike huku mwenye umri mdogo zaidi akiwa mtoto wa miaka miwili na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 77.

Kaunti ya Nairobi iliendelea kuongoza katika visa vya maambukizi mapya ya virusi hivyo ikinakili  visa 77, ikifuatwa na Taita Taveta kwa visa 36, Kiambu iliandikisha visa 20, Busia 9, Kisumu 12 na Meru 11.

Also Read
Madereva watakiwa kuwa makini zaidi msimu huu wa Krismasi

Uasin Gishu na Kilifi zilinakili visa 10 kila moja, Kitui 9, Mombasa 4 huku Laikipia na Muranga zikiandikisha visa 3 kila moja.

Nakuru ilikuwa na visa 2, nazo Machakos, Garissa, Trans Nzoia, Bungoma, Nyamira, Migori, Makueni, Siaya na Vihiga zikinakili kisa kimoja kila moja.

Also Read
Wizara ya Afya yanakili visa 1,463 vya COVID-19 na vifo 26

Kulingana na wizara hiyo ya afya, mgonjwa mmoja wa Covid-19 amefariki na kufikisha idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo hapa nchini 704.

Wagonjwa 664 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku wengine 1,961 wakiwekwa katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi