Visa 506 vipya vya Covid-19 vyathibitishwa hapa nchini

Watu 506 zaidi wamethibitishwa kuambukizwa Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 7,376  zilizochungwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Idadi hiyo mpya inaashiria kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.9.

Katika idadi hiyo mpya watu 468 ni raia wa Kenya huku 38 wakiwa raia wa kigeni.Watu 287 ni wa kiume na 219 ni wa kike. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi miwili na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 103.

Idadi jumla ya visa vya Covid-19 vilivyothibitishwa hapa nchini sasa ni 186,959 huku idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa ikiwa 1,996,442.

Also Read
Watu 392 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kulingana na taarifa ya wizara ya afya, wagonjwa wanane wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo. Mgonjwa mmoja alifariki katika muda wa saa 24 zilizopita huku saba vikiwa vifo vilivyoripotiwa vikiwa vimechelewa katika miezi ya Juni na July. Idadi jumla ya vifo hapa nchini kutokana na Covid-19 sasa ni  3,705.

Wakati huo huo wagonjwa 355 wamepona virusi hivyo hapa nchini ambapo 241 kati yao walikuwa wakitibiwa nyumbani na 114 waliruhusiwa kuondoka kutoka kwa taasisi mbali mbali za afya kote nchini.

Also Read
Raia nchini Uingereza waanza kupokea chanjo dhidi ya Covid-19

Hata hivyo baada ya kukagua rekodi za wizara ya afya katika muda wa miezi 15 iliyopita, watu wengine 45,002 wamebainishwa walipona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini kuwa 174,522 ambapo 138,893 walikuwa wakitibiwa nyumbani na 35,629 walitoka katika hospitali mbali mbali kote nchini.

Also Read
Rais Kenyatta kukutana na Maseneta wa Jubilee Jumanne

Jumla ya wagonjwa 1,128 wamelazwa katika hospitali mbali mbali hapa nchini huku wengine 5,392 wakitibiwa nyumbani.

Wagonjwa 118 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU huku wagonjwa 39 kati yao wakitumia mitambi ya kuwasaidia kupumua, 60 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen na 29 wangali wanachunguzwa.

Hadi kufikia sasa jumla ya watu 1,511,693 wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini. Kati ya idadi hiyo dozi 1,021,982 zilitolewa katika awamu ya kwanza na 489,711 katika awamu ya pili.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi