Visa 571 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Kenya  imenakili kiwango cha maambukizi mapya ya korona cha asilimia 14.4, baada ya watu 571 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi vya korona kutoka kwa sampuli 3,963 zilizopimwa.

Visa hivyo vipya sasa vimeongeza idadi jumla ya maambukizi hapa nchini hadi 45,647.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, waziri wa afya Mutahi Kagwe,alisema tangu kubainishwa kwa kisa cha kwanza hapa nchini mwezi machi,jumla ya sampuli 627,781 zilizopimwa.

Also Read
Kenya yalipiza kisasi kufuatia tangazo la Uingereza kutoruhusu abiria kutoka Kenya

Kati ya visa hivyo vipya,558 ni Wakenya ,ilhali 13 ni raia wa kigeni. 361 ni wanaume na 210 ni wanawake,ambapo mgonjwa wa umri mdogo ana mwaka moja na wa umri mkubwa ana miaka 90.

Wizara ya afya imesema wagonjwa wengine 43 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Kaunti ya Nairobi na Uasin Gishu zinaongoza katika maambukizi mapya kwa visa 116 kila moja, zikifwatiwa na Mombasa kwa visa 74, Kiambu 50, Laikipia 43, Kericho 41, Kisumu 23, Nakuru 21, Busia 16, Trans Nzoia 10, Kajiado 9, Nandi 8 ,ilhali Murang’a, Kilifi na Kirinyaga zimenakili visa vitano kila moja.

Also Read
Watu 36 zaidi wafariki kutokana na COVID-19 hapa nchini

Kaunti za Pokot Mgharibi na Kakamega zimenakili visa vinne kila moja.

Also Read
Wazazi watakaokosa kuwapeleka watoto wao shuleni kuadhibiwa

Wakati uo huo wagonjwa wengine 438 wamepona, 373 chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani na 65 kutoka vituo mbali mbali vya afya hapa nchini.

Idadi jumla ya waliopona sasa imeongezeka hadi 32,522.

Hata hivyo wagonjwa wengine watatu wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo,na kuongeza idadi jumla ya vifo hapa nchini kutokana na korona hadi 842.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi