Visa 618 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Watu 618 zaidi wameambukizwa virusi vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 5,507 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya visa vya Covid-19 vilivyothibitishwa hapa nchini kuwa 193,807. 

Kiwango cha  maambukizi ya virusi hivyo hapa nchini ni cha asilimia 11.1 huku idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa ikiwa 2,064,700.

Kati ya visa hivyo vipya, watu 580 ni raia wa Kenya na 38 ni raia wa kigeni ambapo 333 ni wanawake na  285 ni wanaume. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi sita na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 103.

Also Read
Je wajua kwamba minyoo wa ardhini hutumika kurutubisha udongo?

Kulingana na wizara ya afya wagonjwa 17 zaidi wamefariki hapa nchini kutokana na makali ya Covid-19 huku vifo hivyo vikiwa vile vilivyoripotiwa kuchelewa baada ya ukaguzi wa rekodi za hospitali katika miezi ya Novemba mwaka 2020 na mwezi Machi 2021 na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na Covid-19 kuwa 3,800.

Hata hivyo watu 290 wamepona virusi hivyo huku 261 kati yao wakiruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali kote nchini na 29 wakitoka katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani. Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni watu 183,211 ambapo 46,313 wametoka katika mpango wa kuwatibu wagonjwa nyumbani na 36,898 wakitoka katika viyuo mbali mbali vya afya.

Also Read
Jumba la kilimo lafungwa kutokana na msambao wa Covid-19

Jumla ya wagonjwa 1,222 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini na wagonjwa wengine 4,339 wakitibiwa nyumbani.

Also Read
Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka hadi 39,427 baada ya visa vipya 243 kuthibitishwa

Kupitia kwa taarifa wizara ya afya imesema wagonjwa 139 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo wagonjwa 36 kati yao wanatumia vifaa vya kuwasaidia kupumua na wagonjwa 75 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen. Wagonjwa 29 wangali wanachungwa.

Wakati huo huo watu  1,635,441 wamechanjwa dhidi ya virusi vya Covid-19 kufikia siku ya Jumatatu kote nchini.  Kati ya idadi hiyo watu 1,040,317 walichanjwa katika awamu ya kwanza na  595,124 walichanjwa katika awamu ya pili.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi