Visa 719 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa huku watu 8 zaidi wakifariki hapa nchini

Visa 719 zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 vimenakiliwa hapa nchini na kufikisha idadi jumla ya walioambukizwa ugonjwa huo kuwa 62,488.

Kwenye taarifa, waziri wa afya, Mutahi Kagwe, alisema visa hivyo vipya vilithibitishwa kutokana na sampuli 4,732 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa nchi hii imepima sampuli 742,481 kubaini maambukizi ya ugonjwa huo.

Also Read
Mzozo wa Kenya Uingereza, hasara kwa sekta ya maua

Kati ya visa hivyo vipya, 685 ni vya Wakenya ilhali visa 34 ni vya raia wa kigeni.

Visa 451 ni vya wanaume ilhali visa 268 ni vya wanawake. Mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi mitano ilhali yule mwenye umri mkubwa zaidi ana miaka 81.

Hata hivyo Kagwe alisema watu 8 zaidi wamefariki baada ya kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha jumla ya waliofariki kuwa 1,111 tangu mwezi Machi.

Also Read
Kenya yapokea chanjo zaidi aina ya Johnson and Johnson kukabiliana na COVID-19

Kaunti ya Nairobi iliongoza katika visa hivyo vipya huku ikinakili visa 336, Mombasa  ilikuwa ya pili kwa visa 84 ikifuatiwa na  Busia 50, Kiambu 45, Turkana 33, Kajiado 24 na Kitui 21.

Kaunti ya Nyeri na Garissa  zilinakili visa 20 kila moja, Nakuru 18, Kakamega 17, Mandera 14  na  Machakos 9.

Also Read
Sheria isipotawala, hakuna mtu atakayekuwa salama humu nchini - Maraga

Kilifi, Kirinyaga na Trans Nzoia ziliandikisha visa 4 kila moja, Homabay na Tharaka Nithi  visa 3 kila moja, Nyandarua  na Meru visa 2 kila moja.

Isiolo Kwale , Nyamira, Laikipia , Migori  na Embu zikiwa na kisa kimoja kila moja.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi