Visa 837 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Kenya imeripoti visa 837 vya maradhi ya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 7,545 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Visa hivyo vipya vya maambukizi ni asilimia 11.1 ya maambukizi na vinafikisha idadi jumla ya maambukizi nchini kuwa 191,020.

Kati ya visa hivyo vipya, watu 797 walikuwa wakenya huku 40 wakiwa raia wa kigeni. Mgonjwa mchanga zaidi alikuwa mtoto wa umri wa miezi mitatu huku mkongwe zaidi akiwa na Mzee wa umri wa miaka 94.

Also Read
Mgomo wa wahudumu wa afya kuanza usiku wa manane

Kwenye taarifa, waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa jumla ya wagonjwa 1,058 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku watu 4,407 wakitibiwa nyumbani.

Hata hivyo wagonjwa tisa  wamefariki kutoka na makali ya Covid-19 hapa nchini na kufikisha idadi jumla ya wagonjwa waliofariki kuwa 3,746.

Wagonjwa 340 walipata nafuu ambapo 272 walitoka katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na 68 waliruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali kote nchini. Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 180,420.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 495 huku wagonjwa 19 wakifariki

Wagonjwa 1,058  wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku 4,407 wakitunzwa nyumbani.

Wagonjwa  129 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo 38 Kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na 65 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen. Wagonjwa 26 wanachunguzi

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi