Vituo vinne vya kupima Covid-19 vyawekwa katika kaunti ya Garissa

Serikali ya kaunti ya  Garissa kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu zimeweka vituo vinne vya kupima virusi vya Covid-19 katika eneo hilo.

Naibu mkurugenzi wa huduma za matibabu Ahmed Bashey alisema vituo hivyo vya kupima corona vilivyoko katika gereza la Garissa, shule ya msingi ya Garissa na hospitali ya rufaa sasa vinafanya kazi na viko tayari kwa wananchi wanaotaka kupimwa virusi hivyo.

Also Read
Trump na Mkewe wapatikana na Corona

Akizungumza katika kituo cha kupima covid-19 kilichoko katika shule ya msingi ya Garissa, Bashey aliwahimiza wakazi wa eneo hilo kutembelea vituo hivyo kwa upimaji wa covid-19 bila malipo.

Kwa mujibu wa Bashey serikali ya kaunti ya Garissa imechukua hatua hiyo kufuatia visa vinavyoongezeka vya Covid-19 miongoni mwa wakazi wa sehemu hiyo.

“Katika muda wa saa 72 zilizopita, tumethibitisha visa 5 vipya na hivyo kufikisha idadi jumla ya visa vya Corona katika kaunti ya Garissa kuwa 304 huku visa vya maafa kutokana na virusi hivyo vikifika 10 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo,” alisema Bashey.

Also Read
Watahiniwa 38,797 waliofanya KCPE mwaka 2021 kujiunga na shule za upili za kitaifa

Naibu huyo wa mkurugenzi wa huduma za matibabu alisema kuwa idadi ya sampuli zilizopimwa tangu kuzuka kwa virusi hivyo ni 3,876.

Eneo la Garissa mjini linaongoza kwa visa 238,likifuatiwa na Dadaab kwa visa 51, Fafi  13 huku Lagdera na  Hulugho zikinakili kisa kimoja kila moja.

Also Read
Sonko mashakani huku hoja ya kumbandua ikiwasilishwa katika bunge la kaunti ya Nairobi

Ijara na Balambala hazijanakili kisa chochote.

Hata hivyo Bashey alidokeza kuwa wahudumu wa afya wako katika hatari ya kuambukizwa covid-19 akisema kuwa kati ya wahudumu 497 wa afya waliopimwa virusi hivyo, 45 walithibitishwa kuambukizwa.

Alisikitikia idadi kubwa ya wagonjwa wanaotoroka vituo vya kuwatenga waathiriwa wa Covid-19 akisema wanahatarisha maisha ya wapendwa wao kuambukizwa virusi hivyo.

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Gavana Mandago Sasa ni Seneta

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi