Vituo vya Ajira Digital vyapongezwa kwa kubuni nafasi za ajira kwa vijana

Katibu mwandamizi katika wizara ya teknolojia ya habari, Maureen Mbaka, amepongeza vituo vya Ajira Digital katika eneo bunge la Borabu kwa kuwapa vijana wa eneo hilo fursa ya kujitafutia nafasi za ajira mitandaoni.

Akiongea wakati wa ziara ya ukaguzi wa hatua zilizopigwa na vituo vya teknolojia ya habari kwenye kaunti hiyo, Mbaka aliwapongeza ma-meneja wa  vituo vya Ajira  kw akuwafunza vijana jinsia ya kujitafutia nafasi za ajira.

Also Read
Mpango wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu ustawi wa kiviwanda wazinduliwa

“Kuna mamia ya nafasi za ajira kupitia mtandaoni kwa vijana wa hapa nchini ambazo zitawawezesha kujikimu wakiwa nyumbani. Wanapaswa kutumia fursa hii ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira,” alisema Mbaka.

Also Read
COVID-19: Kenya yaripoti vifo 28 katika muda wa saa 24 zilizopita
Meneja wa kituo cha Ajira Digital cha borabu Fred Ndubi (Aliyesimama)

Mbaka alisema serikali imewekeza fedha nyingi katika miundo msingi ya teknolojia ya habari na kuunganisha huduma za internet kote nchini, na hivyo vijana hawapaswi kutoa vijisababu  vyovyote vya kukosa kupata kazi za mitandaoni  bila kujali mahali wanakloishi.

Mbaka aliwataka ma-meneja wa hao  washawishi wasichana kujifunza jinsi ya kujitafutia kazi za mitandaoni, kwa vile huenda wakajiingzia katika maovu iwapo waatkosa jambo la kufanya.

Also Read
Chama cha FORD-Kenya chatangaza msimamo wa kuunga mkono BBI

Aidha, Mbaka alihimiza vijana wa eneo hilo  kuepukana na desturi ya kuwapsha wanawake  tohara ambvayo bado inaendeelzwa kwenye kaunti ya Nyamira, akioitaja kuwa iliyopitwa na wakati  na ambayo haina nafasi katika jamii ya kisasa.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi