Vyombo vya habari vyamulikwa kwa kujihusisha na michezo ya bahati na sibu

Vyombo vya habari vimetahadharishwa dhidi ya kutumia vituo vyao vya utangazaji kuendeleza michezo ya bahati na sibu isiyo halali.

Baraza hilo limeonya vyombo vya habari dhidi ya kuwatumia vibaya wasikilizaji na watazamani wa vipindi vyao kuendesha michezo hiyo.

Afisa Mkuu wa Baraza la Vyombo vya Habari humu nchini, David Omwoyo, amesema ni kinyume cha sheria kwa vyombo vya habari vilivyo na leseni za kutangaza kujihusisha kwenye michezo ya kubashiri.

Omwoyo ameshtumu tabia ya vyombo vya habari ya kuwataka wasikilizaji na watazamaji wao watume pesa au jumbe huku vikiwaahidi kujishindia pesa.

Also Read
Bunge ladinda kumwondoa Tabitha Mutemi kutoka bodi ya baraza la vyombo vya habari nchini
Also Read
Watu 3 wafariki Mandera baada ya basi walilokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi

Amelalamika kwamba baadhi ya vyombo vya habari hasa vituo vya Redio vinatumia mbinu hiyo kuwapora pesa Wakenya.

“Ni kinyume cha sheria kwa sababu vinajihusisha na michezo ya bahati na sibu ilhali vimepewa leseni ya kutangaza,” amesema Omwoyo.

Omwoyo amesema hayo Mjini Siaya wakati wa kikao cha kutoa ufahamu kuhusu vyombo vya habari kilichohudhuriwa na wanahabari, maafisa wa serikali  na wanachama wa makundi ya kijamii.

Swala la uraibu wa michezo ya bahati na sibu na kamari limeibua utata humu nchini, huku serikali wakati mmoja ikifunga kampuni za mchezo ya bahati na sibu.

  

Latest posts

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,259 vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Walimu watakiwa kuwa mfano bora katika ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi