Vyombo vya habari vyatakiwa kuwajibika katika utoaji wa habari kuhusu Uchaguzi

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna, ametoa wito kwa vyombo vya habari kuripoti matukio kama yalivyo na kujiepusha kuripoti yale ambayo huenda yakachangia taharuki miongoni mwa jamii za humu nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kaunti ya Kisumu Jumatatu asubuhi, Oguna alitaka vyombo vya habari kuwajibika kando na kuonesha uzalendo kwenye kazi zao, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda hali ya amani inayodumishwa nchini kwa sasa.
“Taifa hili ni letu sisi sote vyombo vya habari vikijumuishwa na tunapaswa kulinda amani tunayoshuhudia hapa nchini,” alisema Oguna.

Also Read
Mahakama Kuu yaharamisha utoaji kadi za huduma namba

Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa baraza la vyombo vya habari MCK David Omwoyo alipendekeza mafunzo zaidi na uwezo kwa wanahabari wa humu nchini kwa nia ya kuhakikisha wanaangazia uchaguzi mkuu ujao kwa umakinifu na kwa ufasaha.

Also Read
Zoezi la ukusanyaji saini lang’oa nanga huku Rais Kenyatta akihimiza Wakenya kuunga mkono BBI

Alikariri wito wa umakinifu miongoni mwa wanasiasa wakati wanapotangamana na wanahabari katika kipindi cha uchaguzi akisema baraza la vyombo vya habari halitasita kuwachukulia hatu wanasiasa ambao watawahangaisha waandishi wa habari.

Also Read
Wahudumu wa boda boda watakiwa kuzingatia sheria za barabarani kikamilifu

Wadau katika sekta ya utangazaji walikuwa wamekongamana katika kaunti ya Kisumu Jumatatu asubuhi, kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2022 na kanuni mpya za kuandika taarifa kuhusu uchaguzi.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi