Waakilishi wa Kenya kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa Voliboli ya wanawake,Kenya Prisons na Kenya Commercial Bank wamesajili ushindi wa pili Jumanne mjini Kelibia Tunisia na kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali .
KCB wameilaza Ndejje University kutoka Uganda seti 3-0 za 25-22,25-10 na 25-16 huku Prisons wakijihakikishia nafasi ya kwanza katika kundi C, kufuatia ushindi wa seti 3 kwa bila dhidi ya majirani APR ya Rwanda alama 25-20 katika seti zote.
Mashindano hayo yaliyoanza Mei 19 yatakamilika Juni 24 na yanashirikisha vlabu 16.