Wabunge kurejesha shilingi bilioni 1.2 walizojipatia kinyume cha sheria

Mahakama kuu imewaagiza wabunge warejeshe shilingi bilioni 1.2 ambazo walijipatia kinyume cha sheria kama marupurupu ya nyumba mwaka 2018.

Tume ya mishahara na marupurupu pamoja na mwanaharakati Okiya Omtatah walikuwa wamepinga marupurupu hayo ya shilingi elfu-250  ambazo wabunge hao 416 walijipatia.

Also Read
Tume ya SRC yalaumiwa kwa ubaguzi wa nyongeza ya mishahara

Mahakama ilitaja hatua hiyo ya tume ya kuwaajiri wafanyikazi wa bunge kuidhinisha marupurupu hayo kuwa kinyume cha sheria.

Jopo la majaji watatu limeagiza makatibu wa bunge la taifa na Senate kukata  kiasi hicho kamili kutoka kwa mishahara na marupurupu ya kil mbunge.

Also Read
Chama cha walimu cha KNUT chalaumu kile cha KUPPET kwa kutotetea haki za walimu

Kila mbunge atahitajika kurejesha shilingi milioni- 2.8 kutoka kwa mishahara yao katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Majaji Weldon Korir, Pauline Nyamweya na John Mativo waliamua kwamba tume ya SRC ilitekeleza jukumu lake kwa kuwaagiza makatibu wa mabunge hayo kutolipa marupurupu hayo hatua ambayo haikuingilia uhuru wa kikatiba wa bunge na tume ya kuwaajiri wafanyikazi wa bunge .

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi