Wabunge waliokutana na Ruto wasema marekebisho ya katiba si kipaumbele kwa sasa

Baadhi ya wabunge wamekosoa mswada wa marekebisho ya katiba wakisema haufai, na kwamba umewadia kwa wakati usiofaa.

Wabunge hao waliokutana na Naibu Rais William Ruto nyumbani kwake katika eneo la Karen Jijini Nairobi, wamesema serikali inafaa kuweka kipaumbele shughuli za kufufa uchumi ulioathiriwa na janga a korona nchini badala ya kubadilisha katiba.

Mkutano huo ulilenga kutafakari yaliyomo kwenye mswada wa marekebisho ya katiba chini ya mchakato wa maridhiano wa BBI, ambao umeanza kujadiliwa kwenye mabunge ya kaunti.

Also Read
Isaac Mwaura atimuliwa rasmi Seneti

Baada ya mkutano huo wa faragha wa takribani saa sita, wabunge hao walijitokeza na kukosoa shinikizo zinazoendelea za marekebisho ya katiba.

Wakiongozwa na Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya, mwenzake wa Garrisa Mjini Aden Duale, wa Gatundu Kusini Moses Kuria, Seneta wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen, viongozi hao wamesema mchakato wa marekebisho ya katiba haufai.

Also Read
Naibu Rais William Ruto asema ataendeleza juhudi zake za kuwasaidia wasiojiweza

“Kipaumbele kwa Wakenya sasa ni kuboresha maisha yao, sio mambo ya BBI. Lakini hata kama watalazimisha kwamba watu waangalie mambo ya BBI, Wakenya wapewe nafasi ya kujisomea wenyewe hii BBI wajue nini ambacho watapigia kura,” amesema Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya.

Mkutano huo umejiri huku mabunge ya kitaifa na Seneti yakitarajiwa kurejelea shughuli Jumanne ambapo wabunge wameahidi kushinikiza utekelezaji wa miswada itakayoangazia changamoto zinazowakumba wakulima humu nchini, miongoni mwa maswala mengineyo.

Also Read
Maafisa wa KWS wanasa mashua iliyotekeleza uvuvi haramu Tana River

Wabunge hao pia wamelalamika kuhusu kuondolewa kwa walinzi wao na pia ukosefu wa usalama wa kutosha katika mikutano ya Naibu Rais William Ruto, wakisema hali hiyo inawahatarishia maisha.

Wametoa wito kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kuhakikisha kwamba wanapata ulinzi wa kutosha kulingana na matakwa ya kikatiba.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi