Wafugaji wa Punda Baringo walalamika baada ya kichinjio cha Goldox kufungwa tena

Wafugaji wa Punda katika Kaunti ya Baringo wameshtumu uamuzi wa kufungua upya kichinjio cha Punda cha Goldox katika eneo la Mogotio, wakisema hatua hiyo itaathiri maisha yao.

Kichinjio hicho kilifungwa mwaka mmoja uliopita lakini mahakama iliamua tarehe 15 mwezi uliopita kwamba kifunguliwe tena ili kufanikisha biashara ya nyama na pia ngozi za punda katika masoko ya Bara Asia.

Also Read
Taharuki yatanda Kapedo baada ya afisa wa GSU kuuawa na majambazi
Also Read
Bunge kuanza kujadili mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020

Wafugaji wanadai uamuzi huo ulipendelea wawekezaji, bila kujali wajibu muhimu unaotekelezwa na Punda miongoni kwa jamii za wafugaji wa kuhama hama.

Pia wanadai kwamba bei ya juu ya ngozi za Punda ambazo hutumiwa katika utengezaji dawa huko China imechangia visa vingi vya uwindaji haramu na kwamba huenda wanyama hao wakaangamizwa hivi karibuni.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi