Wafugaji wahimizwa kutumia mbinu za kisasa za ufugaji

Gavana wa kaunti ya Samburu Moses Lenolkulal ametoa wito kwa jamii za wafugaji wa kuhama-hama kuzingatia ufugaji wa kisasa. 

Akiwahutubia wakulima wakati wa siku ya nyanjani katika eneo la  Loibornkare, Kaunti ya Samburu, Gavana huyo alisema kujiwekea mifugo wengi kwa ajili ya kujifurahisha hakutaboresha maisha ya jamii za wafugaji wa kuhama hama.

Also Read
Jeniffer Wambua alinyongwa kwa mikono – Ripoti ya uchunguzi wa maiti

Lenolkulal Alihimiza wakaazi kuzingatia teknolojia ya kisasa ya kilimo ili kujiongezea faida.

Akisema kwamba mifugo wengi ni hatari kwa juhudi za kuhifadhi mazingira, Gavana Lenolkulal alisema mifugo wengi wanafahamika kulemea uwezo wa ardhi katika maeneo kame ya humu nchini-(ASALs) hivyo kudhoofisha maeneo ya malisho.

Also Read
Shule ya Msingi ya Lporos huko Samburu yafungwa kwa hofu ya maambukizi ya Corona

Alihimiza wafugaji kujiwekwa mifugo aina ya Sahiwal na Boran ambao alisena wanastahimili hali ya ukame na kuleta faida kubwa.

Lenolkulal alisema kituo cha uimarishaji mifugo katika eneo hilo kitatumiwa kuboresha uwezo wa wafugaji.

Also Read
Watu wawili wauawa kwa kupigwa risasi Baragoi

Aliyekwua katibu wa wizara Dkt. Richard Lesiyampe aliwahimiza wakulima kutumia mbinu mpya za kilimo ili kujiongezea faida.

Dr. Lesiyampe alisema mifugo wa ki-asili hawataboresha maisha ya jamii za wafugaji wa kuhama hama.

  

Latest posts

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi