Wafugaji wanne wauliwa Turkana huku mifugo 350 wakiibwa

Wafugaji wanne wa mifugo kutoka Turkana jana usiku waliuawa kwa kupigwa risasi na wezi wa mifugo katika eneo la  Nang’usil Ngatuny,Kaunti ndogo ya  Kibish.

Wezi hao wanaoshukiwa kutoka taifa jirani la Ethiopia.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi huko Turkana, Samuel Ndanyi, washukiwa hao wa wizi wa mifugo waliwaua wafugaji wanne na kumjeruhi afisa mmoja wa kikosi cha taifa cha polisi wa akiba, na kuiba mifugo 350.

Also Read
Siku 100 za Jaji Mkuu Martha Koome afisini
Also Read
Serikali haina uwezo wa kuwapima Walimu na Wanafunzi virusi vya Covid-19

Ndanyi alisema afisa wa polisi aliyejeruhiwa anatibiwa hospitalini lakini yuko katika hali dhabiti.

Alisema wafugaji hao na afisa huyo wa polisi wa akiba, walikuwa wakiwaswaga mifugo kwenda kunywa maji  katika mto wa Nakuwa, eneo la  Nang’usil Ngatuny linalopakana na mataifa ya  Kenya na Ethiopia katika Kaunti ndogo ya  Kibish ambapo waliviziwa na wezi hao.

Also Read
Abdalla Mohamed ajiondoa kusailiwa wadhifa wa kamishna wa IEBC

Ndanyi alisema wezi hao wanaaminika  kuwajumwisha watu kutoka makabila ya Toposa na Nyangatom.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi