Wafula Chebukati apinga pendekezo la kuvunjiliwa mbali kwa tume ya IEBC

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC Wafula Chebukati anasisitiza kuwa ili nchi hii iimarishe demokrasia ya uchaguzi mfumo huru wa sasa wa kuwachagua mwenyekiti na makamishna wa tume ya IEBC wapasa kudumishwa.

Kwenye taarifa Chebukati pia amependekeza kuongezwa muda wa kuwaajiri makamishna wa tume hiyo ili kuwapa maarifa yanayohitajika kuhusu shughuli za tume hiyo.

Also Read
Maafisa watatu wa polisi wajeruhiwa baada ya gari lao kushambuliwa Mandera

Kulingana na Chebukati wito unaotolewa kwa sasa wa kutaka kuvunjiliwa mbali tume ya IEBC kwa kuwaondoa makamishna walioko kwa sasa na wafanyikazi utafanya iwe vigumu kuandaa uchaguzi kwa njia shwari.

Alisema kuwafuta kazi wafanyikazi wa tume ya IEBC kunasababisha kupotea kumbukumbu muhimu za tume hiyo na pia kusababisha kuto-kuwepo uthabiti kwenye usimamizi wa uchaguzi.

Also Read
Serikali kujenga maabara ya kuchunguza sumu ya Aflatoxin kwenye nafaka

Chebukati anasema hali kama hiyo husababisha kuto-jiandaa vilivyo kwa uchaguzi na kusababisha mizozo ya kiuchaguzi, hasa matokeo ya uchaguzi wa urais hali ambayo huenda  ikajiri tena kwenye uchaguzi mwaka wa 2022.

Also Read
Mutyambai: Ukiukaji sheria za trafiki ndio sababu kuu ya ajali za barabarani

Kadhalika alipendekeza kukamilishwa kwa marekebisho ya kisheria ya mfumo wa uchaguzi kuambatana na viwango bora vya kimataifa.

Chebukati pia anahimiza kukitwa kwenye katiba hazina ya tume ya IEBC ili kuipa tume hiyo mamlaka ya kusimamia fedha zake.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi