Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i ametoa wito kwa wahasibu kutosita kufichua vitendo vya ufisadi wanavyokumbana navyo wanapotekeleza majukumu yao akisema wanalindwa na sheria dhidi ya yeyote atakayetaka kuwadhuru.

Akiongea mjini Mombasa alipohutubia mkutano wa 39 wa chama cha wahasibu humu nchini Dkt. Matiang’i aliwahimiza wahasibu kutokubali kutumiwa kunufaisha watu wafisadi akisema taaluma yao inawahitaji kuwa waaminifu katika uhasibu wa pesa za umma zinazotumiwa kufadhili maendeleo na utoaji huduma.

Also Read
Serikali yatekeleza mageuzi mapya katika magereza

“Nyinyi ni washirika muhimu zaidi kuhakikisha uwajibikaji wa fedha katika sekta ya kibinafsi. Serikali inawahitaji, lazima msimame kidete na serikali na tutafanya mengi kama taifa,” alisema Matiangí.

Matiang’i alisema taifa hili lina rasilmali za kutosha ambazo zinahitaji kusimamiwa vyema ili kutimiza malengo ya maendeleo ya serikali yanayojumuisha kuimarisha utoaji huduma kupitia uhifadhi, ulinzi na usimamizi bora wa rasilmali hizo.

Also Read
Peres Jepchirchir na Evans Chebet ndio mabingwa wa makala ya 126 ya Boston marathon

Waziri alitoa wito kwa taasisi ya wahasibu wa umma kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na ufisadi kwa kuwafedhehesha wahasibu wafisadi wanaoshirikiana kuiba rasilmali za umma.

Alieleza kufadhaishwa na ongezeko la visa vya ufisadi vinavyowahusisha wahasibu na akakitaka chama cha wahasibu kuwaadhibi wanachama wao wanaohiusika na ufidsadi.

Also Read
Amri ya kuto-toka nje usiku yatangazwa kaunti ya Garissa

Mwenyekiti wa chama hicho George Mokua amesema taasisi hiyo ina wasi wasi kutokana na ongezeko la bei ya vyakula kufuatia ongezeko la bei za kimataifa za mafuta na kutoa wito kwa serikali kuingilia kati suala hilo.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi