Wahudumu wa boda boda watakiwa kuzingatia sheria za barabarani kikamilifu

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna ametoa wito kwa wahudumu wa bodaboda hapa nchini kuzingatia sheria za barabarani.

Kwa mujibu wa Oguna wahudumu wa bodaboda hupuuza sheria za barabarani ambazo wao huziona ni za kuwapotezea wakati lakini huwadhuru baadaye.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na chama cha wahudumu wa bodaboda katika ukumbi wa Tononoka Jijini Mombasa, msemaji huyo wa serikali alidokeza kuwa licha ya sekta hiyo ya uchukuzi wa bodaboda kutoa nafasi nyingi za ajira kwa vijana, imenakili rekodi mbaya ya uzingatiaji sheria za barabarani.

Also Read
Visa 291 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Alitoa changamoto kwa chama hicho cha wahudumu wa bodaboda ambacho kina wanachama milioni 1.4 kutekeleza mafunzo kuhusu usalama barabarani.

Wakati huo huo Oguna aliwahimiza wahudumu hao wa bodaboda kuwekeza katika miradi itakayowasaidia kuboresha hali yao ya maisha.

Also Read
Wafanyibiashara Busia waitaka serikali kuwalipia ada ya NHIF

Oguna alisema kuwa hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu NHIF na chama cha wahudumu wa boda boda nchini, zimetia saini ushirikiano kuimarisha huduma nafuu ya afya  UHC katika kaunti zote 47.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha kitaifa cha wahudumu wa bodaboda   Kevin Mubadi, alisema wanajizatiti kukabiliana na ukosefu wa usalama unaohusishwa na biashara ya bodaboda.

Also Read
Serikali kuimarisha vita dhidi ya awamu ya pili ya uvamizi wa nzige

Afisa mkuu wa hazina ya malipo ya uzeeni NSSF Christopher Kisia aliwahimiza wahudumu hao wa boda boda kujisajili na huduma ya hazina hiyo ya Haba na Haba inayolenga kuwawezesha wanabiashara wadogo wadogo na wale wa kadri.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi