Wakazi wa Baringo wazidi kutoroka kutokana na Utovu wa usalama

Viongozi katika kaunti ya Baringo wamesitisha shughuli zote za kisiasa katika kaunti hiyo hasaa baada ya kuongezeka kwa visa vya utovu wa usalama hali ambayo imefanya wakazi wengi kutoroka makazi yao.

Viongozi hao walisema kuwa hali hiyo inazidi kutatiza amani katika kaunti hiyo na kufanya kuwa vigumu kufanya kampeini za kisiasa.

Also Read
NACADA: Utumizi wa mihadarati umechangia machafuko shuleni

Gavana wa kaunti ya Baringo Stanley Kiptis alikiri kuwa utoaji wa huduma umetatizwa huku majangili wakiendeleza mashambulizi na kuzuia utoaji wa huduma za matibabu katika maeneo muhimu.

Akiwahutubia wanahabari siku ya Jumapili katika kaunti ya  Nakuru, Kiptis alitoa wito kwa serikali ya taifa kuwatuma maafisa wa vikosi vya ulinzi nchini-KDF kusaidia kurejesha usalama katika eneo hilo.

Also Read
Mucheru: Wakenya milioni 1.2 tayari wanafanya kazi chini ya mpango Ajira Dijitali

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Baringo Benjamin Cheboi, alisema kuwa hali ni mbaya zaidi katika eneo hilo huku akitoa wito wa kutolewa kwa misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha kuwa waathiriwa ambao wengi ni wanawake na watoto hawaathiriki hasa na baa la njaa.

Also Read
Magoha: Serikali iko tayari kutekeleza mtaala wa CBC

Cheboi aliongeza kuwa wataanda mkutano mkuu wa vionozi huko Kabarnet baadaye juma hili ili kutafuta suluhu la kudumu kwa masaibu yanayowakumba wakazi wa kaunti hiyo.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi