Wakazi wa Gaza wapokea misaada ya chakula baada ya kusitishwa kwa mapigano na Israeli

Msafara wa kwanza wa malori yaliobeba misaada ya chakula umefika katika ukanda wa Gaza baada ya kutangazwa kwa mkataba wa kukomesha mapigano baina ya Israel na makundi ya Wapalestina.

Maelfu ya Wapalestina wamerejea katika makazi yao yalioharibiwa huku ikidokezwa kuwa itachukua miaka kadhaa kujenga upya makazi hayo.

Also Read
Benjamin Netanyahu ang'atuliwa mamlakani

Shirika la afya duniani (WHO) limetoa wito wa kubuni maeneo maalum ya kuwahamisha majeruhi wa mapigano hayo.

Also Read
Vikosi vya upinzani vyaondoka Jijini Mogadishu baada ya makubaliano ya kisiasa

Zaidi ya watu 250 waliuawa kwenye mapigano hayo ya siku 11, wengi wao wakazi wa ukanda wa Gaza.

Malori ya mashirika mbali mbali ya kutoa misaada yameanza kupeleka dawa, vyakula na mafuta katika ukanda wa Gaza baada ya Israel kufungua kivukio cha Kerem Shalom.

Also Read
Polisi nchini Nigeria waamriwa kukomesha ghasia nchini humo

Zaidi ya watu laki moja walikuwa wametoroka makwao katika ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na kundi la Hamas.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi