Wakazi wa kaunti ya Isiolo wakashifu hatua ya polisi ya kuwaua ng’ombe 200 katika kijiji cha Lobarsherik

Wakazi wa kijiji cha Lobarsherik kilichoko wadi ya Oldonyiro katika kaunti ya Isiolo wameelezea kutamaushwa kwao na oparesheni ya asasi mbali mbali za usalama kufuatia kisa ambapo zaidi ya ng’ombe 200 walipigwa risasi na nyumba kadhaa kuteketezwa.

Kundi la wataalam kutoka sehemu hiyo, limeshtumu oparesheni hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda wa wiki tatu zilizopita huku wakiwashtumu polisi kwa ukatili ambao wanawazuia walishaji mifugi kuwasilisha mifugo katika shamba kubwa la ufugaji la Loisaba lililo ukingo mwingine wa mto Ewaso Nyiro katika kaunti ya Laikipia.

Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Oldonyiro ambaye pia ni naibu spika wa bunge la Isiolo David Lemantile, kundi hilo lilitaja oparesheni hiyo inayoendelea kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za kimsingi za binadamu na za wanyama.

Lemantile alilalamika kuwa ng’ombe hao 200 walipigwa risasi ndani ya kauti ya Isiolo na wala sio karibu na shamba la Loisaba inayomilikiwa na setla mzungu katika kaunti jirani ya Laikipia ambalo linalindwa na maafisa wa polisi.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Isiolo Joseph Kigen, alisema maafisa hao wanawasaka walishaji mifugo waliojihami vikali ambao waliwashambulia maafisa wa polisi katika sehemu ya Loisaba na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi